BAADA ya mapumziko ya wiki mbili, kikosi cha Coastal Union kimerejea mazoezini kujinoa kwa michezo ya ligi iliyo mbele yake huku kocha Mohammed Muya akilia na washambuliaji.
Muya ambaye alijiunga na timu hiyo akichukua mikoba ya Ali Muhammed Ameir, ameiongoza katika mechi mbili akiambulia pointi mbili, kwa sare dhidi ya Mtibwa Sugar ugenini na dhidi ya Fountain Gate nyumbani.
Akizungumza na Mwanaspoti, Muya amesema baada ya kurudi uwanja wa mazoezi ana kazi ya kufanya kwenye eneo la ushambuliaji baada ya kupunguza makosa eneo la ulinzi ambalo amelitaja kuwa lilikuwa na udhaifu baada ya kukabidhiwa timu lakini limepunguza makosa.
“Safu ya ushambuliaji ina upungufu kidogo kwani kwenye mechi mbili nilizosimamia tumefunga bao moja na kuruhusu bao moja tulianza na suluhu na baadae sare hivyo nina kazi ya kufanyia kazi udhaifu ambayo wanayo washambuliaji wangu,” amesema.
“Wachezaji waliopo wana uwezo mkubwa ni makosa madogo madogo ndio yanawagharimu naamini kabla ya kurudi kwa ligi tutakuwa sawa.”
malengo ni kuona tunafunga mambo mengi ambayo yatatuweka kwenye nafasi nzuri.”