Viongozi Wakuu wa CHADEMA Wameachiwa kwa Dhamana – Global Publishers



Viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA): Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara John Heche, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Amani Golugwa, Mwenyekiti Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama Boniface Jacob (Boni Yai) na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Godbless Lema wameachiwa kwa dhamana leo tarehe 10 Novemba 2025

Viongozi hao wanatarajiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam siku ya kesho Novemba 11, 2025 kwa hatua zingine za kisheria.