MAHAKAMA Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imeahirisha kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu hadi Jumatano Novemba 12, 2025 baada ya upande wa Jamuhuri kueleza kuwa Lissu ameshindwa kuletwa kwa sababu za kiuslama.
Mapema leo wakili wa Serikali Mwandamizi, Tawabu Issa akisaidiana na wakili wa serikali Mwandamizi Cathbert Mbilinyi alidai mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru akisaidiana na Jaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde kuwa mshtakiwa Lissu hajaletwa leo na walipofuatilia magereza wameambiwa ni sababu za kiusalama.
“Waheshimiwa majaji, kesi leo ilikuwa inakuja kwa ajili ya kuendelea kusikiizwa, kwa shahidi wa upande wa mashtaka, mshtakiwa Tundu lissu hayupo mahakamani na tumewasiliana na mkuu wa magereza amesema ameshindwa kumfikisha kwa sababu za kiusalama.” Amedai Issa.
Amedai kuwa kesi ilikuwa iendelee na uslilizwaji Novemba 3 na kutokana na hali ha kiusalama kutokuwa imetengemamaa huko nje ikapangwa leo (Novemba 10, 2025) kwa ajali ya kuendelea na usikilizwaji….kutokana na hali ya Dar es Salaam kutokuwa kwenye utulivu pia mashahidi waliopaswa kufika kutoka Mbeya na Ruvuma wameshindwa kufika kwa ajili ya maandalizi ya usikilizwaji wa shauri hili.
Amedai kuwa,kufuatia hali hiyo hawakuwa wamepata shahidi kutokana na hali ya usalama wa jiji la Dar es Salaam kutokuwa salama kwa asilimia 100, hivyo akomba shauri hilo liahirishwe kwa siku 14 chini ya kifungu cha sheria cha 302 (1) cha CPA
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 12, 2025 kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa. Mahakama imewataka upande wa Jamhuri kuhakikisha siku hiyo wanakuwa na shahidi. Pia imetoa hati ya wito kwa mshtakiwa aletwe mahakamani kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa shauri.