Siku moja baada ya Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi kutangaza kuondoa mifarakano na kulileta pamoja Taifa, tayari Viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameachiwa kwa dhamana.
Viongozi hao ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara John Heche, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Amani Golugwa, Mwenyekiti Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama Boniface Jacob (Boni Yai) na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema, dhamana yao umetolewa leo 10 Novemba 2025
Hii inaweza kuwa hatua nzuri kwenye safari ya Maridhiano kama alivyotangaza Dkt. Nchimbi, kuondoa mifarakano na kuleta pamoja taifa, kulinda amani na kurudisha umoja baada ya migawanyiko ya Uchaguzi!?
Heche yeye alikuwa anashikiliwa na Polisi tangu Oktoba 22, 2025, alipokamatwa nje ya geti la Mahakama Kuu Dar es Salaam, alipokuwa akienda mahakamani, kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini.