Na Mwandishi Wetu.
CHAMA cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) kinalaani vurugu, mauaji, na uharibifu wa mali vilivyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Chama hicho pia kinatoa pole kwa wote waliopoteza ndugu au mali na kuunga mkono inaunga mkono agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kufanya uchunguzi wa kina na kuwawajibisha wahusika wote kwa mujibu wa sheria.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa katiba ya 1977 inatambua haki za binadamu kama uhuru wa maoni na maandamano, lakini haki hizo zina mipaka ya kisheria kulinda amani na usalama wa taifa.
” Maandamano ya tarehe 29 Oktoba 2025 hayakuwa halali, kwani yalikiuka zuio la Polisi na kusababisha vurugu,”
“TPBA inasisitiza kuwa matumizi ya nguvu na silaha yanapaswa kuwa ya kiwango cha lazima pekee na kwa uwajibikaji wa kisheria. Kuhusu changamoto za intaneti, mamlaka zinaweza kudhibiti mawasiliano kwa muda kwa mujibu wa sheria kulinda usalama wa taifa.,”ilieleza sehemu ya taarifa hiyo
Pia imeeleza kuwa chama kinakumbusha kuwa haki huambatana na wajibu wa kuheshimu Katiba na mamlaka halali. na kwamba Vyama vya siasa vilivyohusishwa na vurugu vinaweza kufutiwa usajili kwa mujibu wa sheria.
Aidha TPBA inatoa mwito wa utulivu, umoja, na mazungumzo ya maridhiano kama alivyoeleza Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa niaba ya Rais, ili taifa liendelee kuwa mfano wa amani barani Afrika.

