Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Dk Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu. Jina la Dk Mwigulu limewasilishwa bungeni saa 3:06 asubuhi leo Alhamisi, Novemba 13, 2025 na mpambe wa Rais kwa Spika wa Bunge, Mussa Zungu, kisha kusomwa kwa wabunge ambao watamthibitisha kwa kura.
Dk Mwigulu ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi Mkoa wa Singida akipitishwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kassim Majaliwa ambaye ametumikia nafasi hiyo kwa miaka kumi mfululizo, kuanzia mwaka 2015 hadi 2025.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.