………………
Dodoma.
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo Jipya la Chato kusini inapenda kutoa hongera za dhati kwa Mheshimiwa Pascal Lukas Lutandula, kwa kuapishwa rasmi kuwa Mbunge wa Kwanza wa Jimbo la Chato kusini katika Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Novemba 12, 2025 jijini Dodoma.
Kuapishwa kwa Mheshimiwa Lutandula ni hatua muhimu na ya kihistoria kwa wananchi wa Jimbo la Chato kusini, ikiwa ni mwanzo wa safari mpya ya maendeleo, umoja, mshikamano na utumishi wenye dira kwa wananchi wote wa jimbo hilo jipya.
Ofisi ya Mbunge inampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa heshima hii kubwa, na inamtakia mafanikio mema katika kutekeleza majukumu yake mapya ya kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uwazi na ubunifu, sambamba na kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ya kweli ndani ya Jimbo hilo.
Kauli mbiu ya Jimbo la Chato Kusini ni “KAZI NA BATA” hatua hiyo inaakisi mwanga mpya kwa jamii ikihimiza kufanya kazi kwa bidii kisha kupata mapumziko na kupunguza msongo kwa lengo la kujenga jamii iliyostaarabika na yenye maendeleo kwa kila mwananchi.
Imetolewa na:
Daniel Limbe,
Ofisi ya Mbunge – Jimbo la Chato Kusini.