Na Mwandishi Wetu, Babati
Dereva bodaboda wa mjini Babati, Filemon Mbaga, amepewa pikipiki mpya na Kampuni ya Mati Super Brands Ltd baada ya kuibuka mshindi katika challenge ya ubunifu ya kutangaza bidhaa za kampuni hiyo kupitia vyombo vya usafiri.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hiyo, Meneja wa Chapa wa Mati Super Brands Ltd, Isack Piganio, alisema kampuni hiyo ina utaratibu wa kuthamini watu wanaounga mkono bidhaa zake kwa ubunifu katika maeneo yao ya kazi.
“Tumemchagua Filemon kwa sababu ameonyesha ubunifu wa kipekee katika kubandika nembo na picha za Strong Dry Gin kwenye pikipiki na helmeti yake. Tunatambua mchango wake, na pikipiki hii ni sehemu ya motisha kwa kazi nzuri aliyoifanya,” alisema Piganio.Aliongeza kuwa challenge hiyo imekuwa ikitumika kama njia ya kuibua vipaji na kuwapa vijana majukwaa ya kujitangaza na kujiongezea kipato, huku akitaja mfano wa Abdul, dereva wa bajaji aliyewahi kuzawadiwa bajaji mpya katika challenge kama hiyo.
Bidhaa za Mati Super Brands Ltd zinazotajwa zaidi sokoni ni pamoja na Strong Dry Gin, Strong Coffee, Sed Pineapple Flavor Gin, Tanzanite Premium Vodka, Tanzanite Royal Gin na Tai Paa Kibabe, ambazo zimeendelea kupata umaarufu kutokana na ubora wake.
Kwa upande wake, Filemon Mbaga aliishukuru kampuni hiyo kwa kutambua juhudi zake na kusema kuwa zawadi hiyo itakuwa chachu ya maendeleo katika maisha yake.
“Nawashukuru sana kwa zawadi hii. Pikipiki hii itanisaidia kuongeza kipato changu, na ninatarajia kujenga nyumba na kusomesha watoto wangu. Nitaendelea kuwa balozi mzuri wa bidhaa za Mati,” alisema Mbaga.
Uongozi wa Mati Super Brands umeendelea kusisitiza kuwa utashirikiana na vijana wabunifu nchini ili kuwapa motisha katika kutangaza bidhaa za kampuni hiyo sambamba na kukuza fursa za maendeleo.

