Wadau 1,200 kukutana Arusha kujadili Akili Unde Afrika

Dar es Salaam. Takribani washiriki 1,200 kutoka nchi zaidi ya 40 wanatarajia kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Afrika wa Akili Unde ‘AI’ (APAIC2025) katika kuhimiza mageuzi ya kidigitali, ubunifu na maendeleo endelevu.

Mkutano huo utafanyika jijini Arusha katika kituo cha kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kuanzia Novemba 24 hadi 27 mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa APAIC 2025, Abdulwahid Ali Khamis amewaambia wanahabari jana Alhamisi Novemba 13, 2025 mkutano huo, utakuwa wa kihistoria utakaomua pia mustakabali wake katika teknolojia ya akili mnemba.

“Huu ni mkutano wa mwisho wa mwaka kuhusu Akili Mnemba kwa kuichambua ‘A gentic Al’ kwa mageuzi ya kijamii na kiuchumi Afrika.

“Tunatarajia kuhudhuria zaidi ya wajumbe 1,200, wazungumzaji 150, na washiriki kutoka zaidi ya nchi 40,” amesema Khamis.


Khamis amesema mada kuu katika mkutano huo itakuwa  Mapinduzi ya Agentic ‘Al’kuelekea mustakabali wa ubunifu, uhuru na uwezo wa kibinadamu ukilenga kuonesha namna teknolojia Akili Unde inavyo jifunza na kufanya uamuzi kwa uhuru na kuchochea maendeleo ya kijami na kiuchumi.

“Tofauti na mikutano mingine ya teknolojia ,APAIC 2025 imejikita katika matokeo ya vitendo kwa kuunganisha Serikali, matumizi jumuishi, bunifu na yenye uwajibikajI wa Akili Unde katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu kilimo na biashara 

Khamis ambaye piani Mwenyekiti wa APAIC 2025 alisema utawala bora.

“Afrika ipo katika kipindi cha uamuzi mulimu,tunaweza kuendelea kutumia teknolojia kutoka nje au tukaamua kuunda mifumo yetu ya akili unde inayozingatia maadili, takwimu na vipaumbele vyetu vya mandeleo na safari hiyo inaanziahapa Arusha,” amesema.

Khamis amesema mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Scan Code Tanzania, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Costech, HAM International, na washirika wa kimataifa akiwemo kampuni ya Al (Marekani), inayoongoza katika utafiti na ubunifu wa Agentic AL.

Kwa mujibu wa Khamis, katika mkutano huo itashuhudiwa utiaji saini wa Azimio la Mombasa kuhusu Agentic Al, litakaloweka ramani ya pamoja kuhusu utawala wa akili unde uwekezaji na maadili ya matumizi ya takwimu.

Mkurugenzi wa mkutano huo, Anthony Nivo amesema uamuzi wa kuandaa APAIC 2025 jijini Arusha unaashiria kuongezeka kwa nafasi ya Afrika Mashariki kuongoza mageuzi ya kidigitali.