Muheza Watangaza Nafasi 15 za Ajira Mpya Serikalini – Global Publishers



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi kumi na tano (15) za kazi baada ya kupokea kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.


1. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 5

Majukumu ya Kazi

  1. Kuorodhesha barua zinazoingia kwenye rejista.
  2. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi.
  3. Kusambaza majalada kwa watendaji.
  4. Kupokea majalada yanayorejeshwa masijala.
  5. Kutafuta majalada/nyaraka zinazohitajika.
  6. Kurudisha majalada kwenye kabati/shubaka.
  7. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya taasisi.

Sifa za Mwombaji

  • Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
  • Cheti cha Stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
  • Ujuzi wa kompyuta.

Ngazi ya Mishahara

TGS C


2. MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 5

Majukumu ya Kazi

  1. Kuchapa barua/taarifa za kawaida na za siri.
  2. Kupokea wageni na kuwaelekeza.
  3. Kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, ratiba na tarehe za vikao.
  4. Kutafuta majalada yanayohitajika.
  5. Kupokea na kusambaza majalada.
  6. Kukusanya, kutunza na kurejesha nyaraka sehemu husika.
  7. Kuandaa dondoo na maandalizi ya vikao.
  8. Kuandaa orodha ya mahitaji ya ofisi.

Sifa za Mwombaji

  • Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
  • Stashahada/Diploma ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6.
  • Kuandika maneno 100 kwa dakika (Kiswahili na Kiingereza).
  • Ujuzi wa kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher).

Ngazi ya Mishahara

TGS C


3. DEREVA DARAJA II – NAFASI 5

Sifa za Mwombaji

  • Kidato cha Nne (Form IV).
  • Leseni daraja E au C, iliyoitumikia angalau mwaka 1 bila ajali.
  • Cheti cha mafunzo ya udereva (Basic Driving Course) kutoka chuo kinachotambuliwa.

Majukumu ya Kazi

  1. Kukagua gari kabla na baada ya safari.
  2. Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi.
  3. Kufanya matengenezo madogo ya gari.
  4. Kutunza na kuandika log book.
  5. Kusambaza nyaraka mbalimbali.
  6. Kufanya usafi wa gari.
  7. Kazi nyingine zozote atakazoelekezwa.

Ngazi ya Mishahara

TGS B


MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  1. Awe raia wa Tanzania, umri miaka 18–45.
  2. Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kuainisha ulemavu wao kwenye mfumo.
  3. Waombaji wa kada ya Dereva waambatishe vyeti vya mafunzo ya udereva.
  4. Ambatanisha CV yenye maelezo kamili, namba za simu, email na majina ya wadhamini watatu.
  5. Waajiriwa katika nafasi za kuingilia serikalini hawaruhusiwi kuomba.
  6. Ambatanisha vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria:
    • Cheti cha kidato cha IV/VI
    • Cheti cha kompyuta (kama kinahitajika)
    • Vyeti vya kitaaluma
    • Diploma/Certificate/Stashahada nk.
  7. Statement of results, testimonials na results slips HAZITAKUBALIWA.
  8. Waliosoma nje wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU/NECTA/NACTE.
  9. Wastaafu hawaruhusiwi kuomba bila kibali maalum.
  10. Taarifa za uongo zitachukuliwa hatua za kisheria.
  11. Mwisho wa kutuma maombi: 26 Novemba 2025.
  12. Ambatanisha barua ya maombi iliyosainiwa, iandikwe kwa:

Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza
S.L.P. 20, MUHEZA