MAKAMU WA RAIS AKIREJEA NCHINI BAADA YA MKUTANO WA MAZIWA MAKUU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.
Emmanuel Nchimbi, akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Zanzibar Mhe.
Salehe Juma Mussa (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa (kulia) mara baada ya
kumalizika kwa Mkutano wa Tisa wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi
za Ukanda wa Maziwa Makuu (
ICGLR), uliyofanyika,
Jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.
Emmanuel Nchimbi akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa N’djili,
Kinshasa mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Tisa wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (
ICGLR), uliyofanyika, Jijini Kinshasa, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.