Rais Samia Amteua Joel Nanauka Kuongoza Wizara Mpya ya Vijana – Video – Global Publishers



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Joel Nanauka kuwa Waziri wa Vijana, wizara mpya ambayo imeanzishwa kwa lengo la kuimarisha ushiriki na maendeleo ya vijana nchini.

Uteuzi huo umetangazwa leo katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, ambako Rais Samia aliweka wazi kuwa kuanzishwa kwa wizara hiyo kunalenga kuongeza nguvu katika kutatua changamoto za vijana, kukuza ajira, ubunifu, ujasiriamali pamoja na kuongeza ushiriki wao katika maendeleo ya taifa.

Joel Nanauka, ambaye amekuwa akijulikana kwa mchango wake katika masuala ya maendeleo ya vijana, uongozi na uhamasishaji, sasa anapewa jukumu la kusimamia sera na mipango yote inayohusu vijana katika wizara hiyo mpya.

Rais Samia amesema serikali inatarajia kuona mageuzi makubwa kupitia wizara hiyo, ikiwamo kuongeza nafasi za vijana kushiriki katika mifumo ya uchumi na maamuzi ya kitaifa.

Uapisho wa Waziri huyo mpya unatarajiwa kufanyika muda wowote kuanzia sasa.