Dodoma, Tanzania — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza Baraza jipya la Mawaziri leo Jumatatu, Novemba 17, 2025, ambapo baadhi ya mawaziri waliokuwa na nafasi kubwa katika serikali ya awamu iliyopita hawajarejea kwenye baraza hilo.

Miongoni mwa waliotemwa ni vigogo waliokuwa na nyadhifa nzito serikalini, wakiwamo:
-
Dkt. Doto Biteko – aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
-
Hussein Bashe – Waziri wa Kilimo
-
Innocent Bashungwa – Waziri wa Mambo ya Ndani
-
Jenista Mhagama – Waziri wa Afya
-
Dkt. Selemani Jafo – Waziri wa Viwanda na Biashara
-
Dkt. Pindi Chana – Waziri wa Maliasili na Utalii
-
Dkt. Damas Ndumbaro – Waziri wa Katiba na Sheria
Kutemwa kwao kunafanya viongozi hao, ambao bado ni wabunge, kubaki katika nafasi zao za kibunge na hivyo kukaa viti vya nyuma (backbenchers) kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mabadiliko haya katika Baraza la Mawaziri yanakuja wakati Rais Samia akisisitiza kuongeza ufanisi, uwajibikaji na kasi ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Serikali.
STORI NA SIFAEL PAUL, GPL

Related
