JUBILEE INSURANCE WAZINDUA OFİSİ YAO MPYA FAYKAT TOWER

Na Mwandishi Wetu

JUBILEE Insurance (Jubilee Life na Jubilee Health) leo Novemba  17,2025 wamezindua rasmi ofisi yao mpya iliyopo ghorofa ya tatu jengo la Faykat Tower. 

Uzinduzi wa ofisi hiyo mpya ni muendelezo wa ahadi yao ya kuendelea kutoa huduma bora za bima ya Afya na bima ya Maisha kwa Watanzania.

Taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo imesema kwamba Jubilee Insurance inawakaribisha mawakala na wateja wake kutembelea ofisi hizo kwa msaada zaidi kuhusu maswala ya bima.

Katika uzinduzi huo mbali ya kuhudhuriwa na waalikwa mbalimbali pia alikuwepo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jubilee Health Insurance Dk.Harold Adamson pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jubilee Life Insurance Bi. Helena Mzena.