Sababu zatajwa tovuti, aplikesheni kushindwa kufanya kazi duniani

Dar es Salaam. Baadhi ya tovuti duniani (website), pamoja na aplikesheni kama  X, PayPal na ChatGPT leo Jumanne zimepitia changamoto ya kushindwa kufanya kazi kutokana na hitilafu iliyojitokeza kwenye miundombinu ya intaneti ya kampuni ha Cloudflare. 

Cloudflare ni kampuni inayosaidia tovuti kulinda na kudhibiti trafiki ya intaneti. Kazi kuu ya Cloudflare ni kusaidia kulinda na kuharakisha rasilimali za intaneti. 

Ilianzishwa mwaka 2009 kwa lengo la kudhibit barua taka (email spams) lakini Imebadilika na leo inahudumia mamilioni ya watumiaji kwa kutumia DNS na huduma za usalama.

Cloudflare leo imesema tatizo lilianzia saa 6:30 asubuhi likisababishwa na faili la mipangilio (setting file), lililotengenezwa ki-otomatiki kwa ajili ya kudhibiti vitisho vya kiusalama.

Imeelezwa faili hilo lilikuwa kubwa kupita kiasi na kusababisha mfumo wa kushughulikia mtiririko wa data kuanguka, jambo lililosababisha huduma kadhaa kushindwa kufanya kazi.

Katika changamoto hiyo baadhi ya watumiaji wameshindwa ikiwemo kufungua website kwani wamekutana na ujumbe wa Cloudflare error.

Ujumbe uliokuwa unajitokeza ukifungua apps au tovuti mbalimbali ulikua unasema “Please unblock challenges.cloudflare.com to proceed”. Wengine wakipokea jumbe za Error wakati wanaperuzi mitandaoni.

Kwa sasa mtandao huo umerudi kawaida watu wanaweza kutumia apps au tovuti mbalimbali kama kawaida kwani Changamoto hiyo ilijitokeza kuanzia mida ya asubuhi mpaka jioni imetatuliwa.
 
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya kiteknolojia: “Cloudflare wanafahamu, na wanachunguza suala hilo kwa undani ambalo halijaathiri wateja wengi.

Hata hivyo kampuni hiyo imehahidi baadhi ya mifumo itaendelea kupata changamoto huku ikijitahidi kutatua matatizo ya kiufundi yanayowakabili.

Ikumbukwe changamoto hii inakuja ikiwa ni mwezi unepita tangu kukatika kwa huduma za wavuti za Amazon ambapo tovuti na programu zaidi ya 1,000 zikikatika nje ya mtandao.

Mtoa huduma mkuu wa huduma za wavuti, Microsoft Azure, pia aliathiriwa muda mfupi baadaye na tatizo hilo.