Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa serikali yake imekubali kuiuzia Saudi Arabia ndege za kivita za kisasa aina ya F-35, hatua inayokuja kabla ya mkutano wake Ikulu ya White House na Mwanamfalme Mohammed bin Salman.
Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya mazungumzo hayo, Trump alisema:
“Tutafanya hivyo. Tutawauzia ndege za F-35. Amekuwa mshirika mzuri.”
Mazungumzo Yaangazia Ulinzi na Nishati ya Nyuklia
Mazungumzo kati ya viongozi hao yanatarajiwa kugusia makubaliano ya ulinzi, matumizi ya nishati ya nyuklia ya kiraia, pamoja na masuala mapana ya ushirikiano wa kijeshi. Ziara hii ya Jumanne ndiyo ziara ya kwanza ya kiongozi mkuu wa Saudi Arabia kuitembelea White House tangu mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi mwaka 2018.
Kivuli cha Mauaji ya Khashoggi Charejea
Ripoti ya kijasusi ya Marekani ilionyesha kuwa Mwanamfalme Mohammed aliidhinisha operesheni iliyosababisha kuuawa na kukatwa vipande kwa mwandishi Jamal Khashoggi ndani ya ubalozi wa Saudia nchini Uturuki.
Hata hivyo, Mwanamfalme amekanusha mara kadhaa kuhusika na mauaji hayo, akisema hakutoa agizo lolote lililosababisha tukio hilo.
Related
