TUMEMKAMATA DKT KIBABA KWA TUHUMA ZA JINAI

……………

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limemkamata na linaendelea kumhoji Dkt. Kibaba Furaha Michael, Mkazi wa Manispaa ya Geita.

Limeeleza sababu za kumkamata ni kutokana na ushahidi uliokusanywa ambao umehusiana na tuhuma mbalimbali za kijinai anazotuhumiwa nazo.

Jeshi Hilo limeeleza Uchunguzi uliobakia unakamilishwa ili hatua zinazofuata za sheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake na anao shirikiana nao.