MAKAMU WA RAIS AWASILI NCHINI ZAMBIA KUSHIRIKI UWEKAJI JIWE LA MSINGI UKARABATI WA RELI YA TAZARA

……………………

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt.
Emmanuel Nchimbi amewasili Jijini Lusaka nchini Zambia leo Novemba 19, 2025.

Makamu wa Rais anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la
Msingi la Uzinduzi wa Ukarabati Mkubwa wa Reli ya TAZARA itakayofanyika tarehe
20 Novemba 2025 Jijini Lusaka.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Makamu wa Rais
amepokelewa na Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Dkt. Elijah Muchima,
Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Balozi, Luteni Jenerali Mathew Mkingule,
Maafisa waandamizi wa Jamhuri ya Zambia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja
na vikundi mbalimbali vya ngoma vilivyoandaliwa kwa heshima yake.

Pamoja na viongozi wengine, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Nchimbi ameambatana
na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara, Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Masanja pamoja Mkurugenzi Mkuu
TASAC Bw. Mohamed Salum.