NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Mchezaji wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans na timu ya Taifa ya Tanzania, Clement Mzize amefanikiwa kuchukua tuzo ya goli bora la mwaka la shirikisho la soka barani Africa CAF.
Goli hilo alifunga kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya Makundi katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.