AGN yaongoza mawaziri nane wa Afrika kuzungumza na UN kuhusu athari za mabadiliko ya tabia ya nchini katika mkutano wa COP30, Brazil


KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres (kulia), akizungumza na Mjumbe Maalum na Mshauri wa Rais kuhusu Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Majadiliano la Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (AGN), Dkt. Richard Muyungi, aliyekuwa akiongoza ujumbe wa mawaziri wanane wa Afrika kuwasilisha misimamo ya bara hilo katika majadiliano yanayoendelea kwenye mkutano wa COP30 uliofanyika Belem, Brazil, leo.