Farida Mangube, Morogoro
Zoezi la kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Umeya na Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro kwa tiketi ya chama Cha Mapinduzi (Ccm) limefunguliwa leo huku mwandishi wa Habari wa Gazeti la Uhuru mkoa wa Morogoro Latifa Ganzeli akichukua fomu ya kuwania unaibu meya wa Manispaa ya Morogoro.
Akizungumzia zoezi hilo,Katibu wa Umoja wa Vijana(UVCCM)Wilaya ya Morogoro mjini Khalid Hossein King amesema kuwa zoezi Hilo linatarajiwa kukamilika Novemba 21 majira ya saa kumi jioni huku muitikio ukiwa mkubwa kwa wanachama waliojitokeza kuchukua fomu hizo.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea Unaibu Meya wa Manispaa ya Morogoro,Diwani wa Viti maalumu ambaye pia ni mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru,Latifa Ganzeli amesema kuwa baada ya kulitumikia baraza la Madiwani kwa muda wa miaka 10 ameona sasa ni wakati muafaka wa kugombea nafasi hiyo huku kipaumbele chake kikubwa kikiwa kwenda kuongeza vyanzo vipya vya mapato.

