TAMTHILIA YA NICE TO MEET YAMDONDOSHA TUSA MSIMU WA PILI

WADAU wa Filamu nchini wanapaswa Kupewa moyo kwa Watayarishaji kuhakikisha wanatengeneza Kazi zenye Viwango na weledi ili kuendelea kulipa hadhi soko la filamu Kimataifa na Kunyanyua vipaji mbalimbali.

Akizungumza kauli hiyo Msanii chipukizi ambae pia ni ingizo jipya Munirah pendeza marufuku kama Tusa ndani ya filamu ya “Nice to Meet you “amesema Kwa sasa Wadau wa Filamu wamekuwa na motisha ,hamasa na morali kutengeza kazi nyingi na zenye mvuto hivyo ni wakati wa wasanii kufanya vizuri .

Hata hivyo “Tusa” amewaomba Mashabiki kukimbilia ofa ya Msimu huu wa Sikukuu kuhakikisha wanalipia ving’amuzi vyao vya Startimes ili waweze kupata maudhui mbalimbali ikiwemo tamthilia pendwa ya “Nice to Meet you, katuni ya watoto ya Bonnie bears maarufu kama kipara mbabe pamoja na Super Wings na Maudhui mengine ya Kimichezo na tamthilia zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.

Kwa Upande wake Meneja wa Startimes David Malisa amesema Startimes Wamezindua kampeni hiyo ya “lipa tukubusti” ambayo ni ofa ya kwa wateja wake wote wa Dishi pamoja na Antenna.

“Mteja anapolipia kifurushi cha mwezi mzima basi ana bustiwa kwenda kifurushi cha juu kwa mwezi mzima bure kabisa,Lipia NYOTA mwezi – 11,000 tukubusti mpaka MAMBO – 17,000 na Vifurushi vingi hivyo hivyo huku Vifurushi vikubwa kuongezewa Siku 5

Hata hivyo Malisa ameongeza kuwa Ofa hiyo Mahsusi Kwa Kipindi hiki cha Sikukuu ili kuweka karibu familia hususani watoto ambapo zipo katuni kwa lugha ya Kiswahili ndani ya King’amuzi cha Startimes.