Mwanamfalme wa Saudi Arabia Amuomba Trump Kumaliza vita Sudan – Global Publishers



Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman.

Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan. Hii ni kufuatia ombi la mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman.
Wakimbizi wakipiga gumzo katika kambi huko Tawila

Vita vya Sudan vimeauwa makumi ya maelfu ya watu na kusababisha karibu milioni 12 kupoteza makazi tangu vilipozuka Aprili 2023.

Trump amekemea kile alichokiita “ukatili mkubwa” katika mgogoro ambao aliupuuza hapo awali. Alikiri kuwa vita vinavyoendelea kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF havikuwa kwenye orodha yake, kabla ya kiongozi huyo wa Saudia kumsukuma kuingilia kati.

Lakini Trump alisema sasa atafanya kazi ya kuutuliza mgogoro huo kwa ushirikiano na madola ya kikanda, ikiwemo Umoja wa Falme za Kiarabu, ambao unakanusha tuhuma za kuwaunga mkono RSF kwa kuwapa silaha na mamluki.

Saudi Arabia inaiunga mkono serikali inayoegemea upande wa jeshi. Trump alitoa kauli hizo katika jukwaa la kibiashara na mwanamfalme wa Saudia, siku moja baada ya kumkaribisha katika Ikulu ya White House. Vita vya Sudan vimeauwa makumi ya maelfu ya watu na kusababisha karibu milioni 12 kupoteza makazi tangu vilipozuka Aprili 2023.

Stori na Elvan Stambuli – Global Publishers