NA VICTOR MASANGU, KIBAHA.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijiji Homoud Jumaa ameahidi kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa vitendo ikiwemo kusimamia suala zima la kuwahudumia wananchi ipasavyo katika mambo mbali mbali kwa ajili ya kuwaletea chacu ya maendeleo katiika nyanja tofauti.
Jumaa ameyabainisha hayo wakati wa halfa fupi ya kumpokea rasmi kutokea Mkoani Dodoma ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kuapishwa rasmi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini ambapo sherehe hiyo imehudhuliwa na na viongozi wa chama cha mapinduzi, wananchama pamoja na wananchi kutoka maeneo tofauti.
Mbunge huyo amesema kwamba kwa sasa uchaguzi umeshamalizika na kwamba kitu kikubwa amewaomba wanachama wote na wananchi kuhakikisha kwamba wadumisha hali ya amani na utulivu wa nchi na kuepukana na vurugu ambazo hazina maana na badala yake washikamane katika kukijenga chama pamoja na kushiriki kikamilifu katika mambo ya kimaendeleo.
“Nawashukuru kwa dhati viongozi wangu wa chama cha mapinduzi, wanachama wa ccm pamoja na wananchi wote kwa kuweza kuniamini kwa mara nyingine na kuweza kunipitisha tena kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kitu kikubwa ambacho ninaweza kuwaahidi ni kuendelea kutoa ushirikianio wa hali na mali katika kuhakikisha ninawaletea maendeleo mbali mbali,”amesema Jumaa.
Katika hatua nyiingine Mbunge huyo amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. kwa kuweza kuchaguliwa kwa kishindo pamoja na kuweza kutoa hotuba yake nzuri ambayo imelenga kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi katika sekta mbali mbali.
Kwa upande wake Diwani mteule wa kata ya Kwala Mansuri Kisebengo amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini kwa kuweza kuchaguliwa kwa kishindo na wananchi na kwamba ana imani kubwa wataweza kuwatumikia wananchi na kuwaletea chachu ya maendeleo.
Nao baadhi ya wananchi ambao wamepata fursa ya kuhudhulia katika halfa hiyo wamesema kwamba wana imani kubwa na serikali mpya ya awamu ya sita pamoja na kumpongeza Mbunge wa Jimbo hilo la Kibaha vijijini Hamoud Jumaa kwani ataweza kuleta mafanikio ya kimaendeleo kwa wananchi wake.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijni Mhe. Hamoud Juma amepokelewa kwa kishindo kikubwa na viongozi CCM, wananchama pamoja na wananchi sambamba na madiwani mbali mbali za Jimbo la KIbaha vijijini.
