DKT MAPANA ATEULIWA N/KATIBU MKUU MAENDELEO YA VIJANA

……………

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wawili (2). 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Dkt. Kedmon Elisha Mapana, ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana.

 Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Mapana alikuwa Katibu Mtendaji, Baraza la Sanaa la Taifa  (BASATA).