Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 20 Novemba 2025 amepokea Kitabu Maalum chenye mkusanyiko wa habari picha za kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar 2025.
Kitabu hicho kimekabidhiwa na Mkurugenzi wa Tahsil Solutions, Bw. Benny Kisaka, aliyewasili Ikulu Zanzibar kwa ajili ya kukikabidhi rasmi kwa Rais Dkt. Mwinyi.
Akizungumza mara baada ya kukipokea kitabu hicho, Rais Dkt. Mwinyi amempongeza Bw. Kisaka kwa ubora, umakini na weledi mkubwa uliotumika katika kuandaa na kukusanya taarifa zilizomo ndani ya kitabu hicho, akibainisha kuwa kazi hiyo ni ya thamani katika kuhifadhi historia ya kampeni za uchaguzi.
Kwa upande wake, Bw. Kisaka amesema Kitabu hicho kitaanza kusambazwa katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar kwa lengo la kuifikisha taarifa hiyo kwa umma na kuhakikisha historia hiyo muhimu inabaki kumbukumbu ya vizazi vijavyo.