IAA kuja na tafiti zitakazo saidia kutatua changamoto za kijamii

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof Eliamani Sodeyeka, amesema chuo hicho kimejipanga kuja na tafiti zitakazo saidia kuleta matokeo chanya katika jamii ambazo zitafanywa na wanafunzi.

Aidha amesema baada ya tafiti hizo kufanyika zitajadiliwa kwa pamoja na wanafunzi wengine na kwamba pia zinaweza kusaidia kitaifa kwa kushauri mabadiliko ya kisera ambayo yatachochea ukuaji wa kiuchumi nchini.

Prof. Sodeyeka ameyasema hayo Leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na wanafunzi hao katika mkutano wa pamoja kwa lengo la kuwasilisha tafiti zao (publication) na kuzijadili kwa pamoja.

“Mwananfunzi anapoanza kufanya tafiti ambayo itabidi aitete mbele ya hadhira hiyo itampelekea kuongeza bidii kwa kufanya kazi kwa weledi na ubunifu.

“Lakini kama chuo unapokuwa na tafiti nyingi zenye ubora zinafanya chuo chako kitambulike zaidi kimataifa” amesema Prof Sodeyeka

Meneja Chuo cha Uhasibu Arusha Kampasi ya Dar es Salaam, Dkt. Kelvin Njunwa  amesema lengo la mkutano huo ni kutoa nafasi kwa wananfunzi wa ‘masters’ wanaotarajia kuhitimu mwezi ujao kujadili tafiti walizofanya kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii na kuzifanyia kazi.

Aidha amesema chuo hicho pia kinatoa mafunzo kwa njia mtandao akisisitiza ni fursa kwa watumishi wasio na nafasi kujiendeleza zaidi kielimu.

Mwanafunzi katika chuo hicho anayesoma ‘masters’ ya HRM, Consolata Asenga amesema uwepo wa teknolojia inayowawezesha kusoma kwa njia ya mtandao na kuhitimu ni hatua kubwa katika kufikia mafanikio ya kielimu na matumizi ya mifumo ya kiteknolojia.

 Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho katika mkutano kwa lengo la kuwasilisha tafiti zao (publication) na kuzijadili kwa pamoja, leo Novemba 21, 2025 Jijini Dar es Salaam

Meneja Chuo cha Uhasibu Arusha Kampasi ya Dar es Salaam, Kelvin Njunwa akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho (hawapo Pichani).