KATIKA kudhihirisha kuwa teknolojia inabadilisha maisha ya Watanzania, Jukwaa la Kidijitali la PIKU limeendelea kutoa tabasamu kwa watumiaji wake baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi zikiwemo bodaboda, televisheni aina ya LG, simu mpya aina ya Samsung 06, manukato mbalimbali pamoja koponi za safari za Bolt.
Washindi hao wamekabidhiwa zawadi zao hizo na viongozi wa Jukwaa hilo la Piku huku simulizi zao zikionesha namna bidhaa hizo zitakavyoweza kuwainua na kujikwamua kiuchumi.
Jackson Ngonji ni mshindi wa Pikipiki maarufu bodaboda aina ya TVS HLX 125 anasema ushindi huo utakwenda kubadilisha maisha yake kwani atakitumia chombo hicho cha usafirishaji na kujipatia kipato cha uhakika kila siku na kujikwamua kiuchumi.
Amesema bodaboda hiyo itamsaidia kujitegemea zaidi, kupunguza changamoto za kifedha na hata kuweka akiba kwa ajili ya familia yake kwani ataitumia kufanyia biashara ya usafirishaji wa abiria.
Amesema anaishukuru Piku kwa kuleta jukwaa hilo la kidijitali ambalo linawapa fursa watanzania wakiwemo vijana kubadilisha maisha yao ya kujiajiri.
“Kwa kweli bodaboda hii ni baraka kubwa kwangu, na naahidi kuitumia kwa nidhamu, bidii na ubunifu ili kuendelea kusonga mbele kimaisha, niwashauri watu kujitokeza kucheza katika mnada huu kwani ni wa kweli na hakuna longolongo.” amesema
Naye Nestory Augustine ambaye ni mshindi wa televisheni aina ya LG, router kutoka Airtel na simu aina ya Samsung 06 anasema kupitia bidhaa hizo zitamwinua kiuchumi na kwamba atatumia mtandao na simu kufanya biashara na kujiingizia kipato.
Amesema alihifahamu Piku kupitia mtandao wa Instagram na kwamba alipoona watu wanashinda ndipo na yeye alishawishika kuingia katika mnada huo.
“Nawashauri vijana wacheze mnada huu ni wa kweli kabisa. Ukicheza kwa nia njema utashinda. Mimi ni mara yangu ya kwanza na nimeshinda, nimepata vitu ambavyo nikivitumia vizuri vitanikwamua kiuchumi, nimefurahi sana kwani televisheni hii itaniwezesha kuangalia vitu mbalimbali ikiwemo mipira,” amesema
Aidha washindi wengine katika mnada hu oni Irene Lyimo ambaye amejishindia koponi ya safari ya bolt yenye thamani ya Sh. 100,000, Jonathan Paul ambaye amejishindia simu aina ya Samsung 06 pamoja na Angela Joseph aliyejishindia kombo la kike na kiume pamoja na simu janja aina ya Samsung 06.
Washindi hao wote waeleza kufurahishwa kwao na ushindi huo na kwamba bidhaa hizo walizozipata zimewapa hamasa kubwa kwao na marafiki zao kwa karibu kuamini katika fursa zinazoletwa na teknolojia.
Naye Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Piku Afrika, Barnabas Mbunda amesema minada inayoendeshwa katika jukwaa hilo ni ya kweli na uwazi na kwamba wanataka kuona watanzania wakiwemo vijana na wafanyabiashara wanajipatia bidhaa bora na za kisasa.
“Tunasisitiza kuwa huu si mchezo wa kubahatisha bali ni jukwaa la kidijitali ambalo limetengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu, niwaombe muendelee kushiriki. Usiogope kujaribu mara ya kwanza unaweza kukosa, lakini mara ya pili unaweza kuandika historia ya kujipatia bidhaa za kisasa. PIKU ni yako, ni ya wote, na kila siku tunazidi kuongeza bidhaa mpya,” amesema Mbunda
.jpeg)
