MWENYEKITI WA BODI AIPONGEZA TPA KWA UWEZESHAJI CHUO CHA BANDARI

 

Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhe. Balozi na IGP Mstaafu Ernest J. Mangu akitoa hotuba yake kwenye Sherehe za Mahafali ya Ishirini na Nne (24) ya Chuo cha Bandari Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhe. Balozi na IGP Mstaafu Ernest J. Mangu akikabidhi cheti kwa mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yake katika Mahafali ya Ishirini na Nne (24) ya Chuo cha Bandari Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo cha Bandari Dar es Salaam, Dkt. Lufunyo Hussein, akizungumza katika mahafali hayo, ambapo jumla ya Wahitimu 757 wamemaliza masomo yao.

Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TPA, Bw. Mbarikiwa Masinga akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mkeli Mbossa kwenye mahafali hayo.
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhe. Balozi na IGP Mstaafu Ernest J. Mangu akikabidhi cheti kwa mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yake katika Mahafali ya Ishirini na Nne (24) ya Chuo cha Bandari Dar es Salaam.

MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa

Bandari Tanzania (TPA), Mhe. Balozi Ernest Mangu (IGP Mstaafu); ameipongeza Menejimenti ya TPA kwa uwekezaji mkubwa walioufanya katika Chuo cha Bandari Dar es

Salaam.

Mhe. Balozi Mangu ametoa

pongezi hizo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwatunuku vyeti Wahitimu wa Mahafali ya 24 ya Chuo cha Bandari Dar es Salaam.

Alisema

TPA imekiwezesha chuo hicho kwa kufunga jumla ya mashine kumi (10) ‘simulator’ za kisasa ambazo zinatumika kufundisha masuala anuai, ikiwemo

mafunzo yanayohusisha uchimbaji wa mafuta na gesi.

“Natambua na kupongeza Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari

Tanzania (TPA) kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa katika mwaka wa fedha 2024/2025 katika

chuo hasa kwa kuboresha mazingira ya utoaji mafunzo kwa kuongeza vifaa vya

kufundishia na kujifunzia.”

“…Mipango ya

Serikali ya kuendeleza Bandari za Dares Salaam, Bagamoyo, Tanga, Mtwara na zile

za maziwa pamoja na kufungamanisha Bandari Kavu, Reli na Barabara, itachochea

ukuaji wa biashara katika sekta hii kwa asilimia kati ya asilimia tano (5%)

hadi tisa (9%) kwa mwaka na kufungua fursa za ajira kati ya 80,000

hadi 120,000 za moja kwa moja na za muda katika kipindi cha miaka mitano

ijayo. Kwa wahitimu wa leo hii ni fursa kubwa kwani ajira hizi zinahusiana na

maarifa na ujuzi mlioupata kutoka katika Chuo hiki,” alisisitiza Mhe. Balozi Mangu ambaye alikuwa mgeni rasmi

katika mahafali hayo.

Awali akizungumza katika mahafali hayo, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mkeli Mbossa; Mkurugenzi Rasilimali

Watu na Utawala, Bw. Mbarikiwa Masinga alisema TPA chini ya Wizara ya Uchukuzi itaendelea kuimarisha

huduma za Chuo ziweze kuendana na mabadiliko mbalimbali ya Sera za Nchi.

Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhe. Balozi na IGP Mstaafu Ernest J. Mangu (katikati) akishauri jambo alipokuwa akitembelea moja ya vyumba vya mitambo ya kisasa yakufundishia wanafunzi, kabla ya Sherehe za Mahafali ya Ishirini na Nne (24) kuanza rasmi.
Moja ya mtambo wa kisasa wa kufundishia wanafunzi, ukioneshwa kwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mahafali ya Ishirini na Nne (24) ya Chuo cha Bandari Dar es Salaam.

Aidha alibainisha kuwa uimarishaji wa sera ya

ushirikishwaji wa Sekta binafsi katika uendeshaji na uendelezaji wa Sekta ndogo

ya Bandari unafanywa ili kuendana na dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2050 na

mipango mingine ya Serikali ambayo inaonesha bayana umuhimu na upekee wa sekta

ndogo ya bandari katika uchumi, ajira na mapato ya nchi.

Aliongeza kuwa uboreshaji mafunzo yanayotolewa

na Chuo utawaongezea Wahitimu utaalamu na kujiamini katika kutafuta fursa za

ajira na katika majukumu yao mengine ikiwa ni pamoja na kutoa Rasilimali Watu yenye

sifa na Vigezo vinavyotakiwa katika utekelezaji wa shughuli za miradi mikubwa

ya kimkakati ya Serikali.

“…Napenda kurejea maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoyatoa siku ya uzinduzi wa Bandari Kavu

Kwala kwamba  “ …..Maboresho ya

bandari nchini yaendane na maboresho ya Chuo cha Bandari…..”.

“Nitumie fursa kueleza kwamba mimi

binafsi pamoja na Menejimenti ya TPA ninayoiongoza, tutaendelea kufanya mageuzi

makubwa katika sekta ya bandari na pia kukiboresha Chuo cha Bandari kwa

kukipatia Miundombinu ya kisasa, vifaa na mitambo ya kufundishia, mifumo ya

TEHAMA,  kuajiri watumishi  wapya wenye  sifa zinazotakiwa pamoja na kuendeleza waliopo

waendane na kasi ya mageuzi katika sekta,” inaeleza taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Mbossa.