ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MBEYA KWA TUHUMA ZA KIJINAI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Awali ya “Saint Clemence” ndugu Clemence Kenani Mwandambo, mkazi wa Uzunguni “A” Jijini Mbeya kwa tuhuma za uchochezi.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo Novemba 21, 2025 saa 5:20 asubuhi maeneo ya Uzunguni Jijini Mbeya akitoa na kusambaza maneno ya uchochezi na uchonganishi kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii za “Facebook” na “Instagram”Upelelezi unakamilishwa ili hatua nyingine za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.