Rais Samia atunuku kamisheni maofisa 296

Monduli. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan, amewatunuku kamisheni maofisa wapya 296 katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) kilichopo Monduli, mkoani Arusha.

Rais Samia ametunuku kamisheni hizo kwa maofisa hao leo Jumamosi Novemba 22, 2025 ambapo kati ya hao, maofisa 106 wametunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya kijeshi waliyoisoma kwa miaka mitatu.

Wengine kati ya maofisa hao katika cheo cha Luteni Usu, ni wa kundi la 72/24- Regular (79), marubani 22 na 89 wamepata mafunzo kutoka nchi rafiki.


Kabla ya kuwatunuku Kamisheni, Rais Samia amekagua gwaride lililoandaliwa na maofisa wanafunzi hao na ametoa zawadi kwa wale waliofanya vizuri katika makundi yote.

“Niwapongeze kusimamia mafunzo kwa wanajeshi ili kuhakikisha kuwa yanakuwa na ubora wa hali ya juu utakaowezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Mafunzo haya ni muhimu kwa jeshi letu na taifa kwa ujumla,” amesema.

Aidha, amesisitiza kuwa mafunzo wanayopata maofisa hao ni mhimili muhimu kwa uimarishaji wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania pamoja na ustawi wa taifa kwa ujumla.


Awali, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Rhimo Nyansaho alisema wizara itaendelea kuhakikisha inaongeza idadi ya wahitimu wanawake, huku akiweka bayana kuwa maofisa hao wako tayari kulitumikia taifa kwa ujasiri na uaminifu katika kulinda amani na usalama wa nchi.

Alifafanua kuwa huu ni mwaka wa tatu tangu chuo hicho kianze kujisimamia katika utoaji wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kijeshi.


Amesema Wizara itaendelea kuchukua hatua mahsusi kuhakikisha idadi ya wanawake inaongezeka katika kila mahafali. Alitolea mfano kuwa wakati wa mahafali ya nne na tano kulikuwa na wanawake 21, ilhali mwaka huu idadi hiyo imeongezeka hadi 25, huku wanaume wakiwa 81.

“Mwaka huu tumefikia 25. Ingawa ongezeko hili ni dogo, Wizara inaendelea kuhakikisha idadi ya wahitimu wanawake inaongezeka mwaka hadi mwaka ili kuimarisha uwiano wa kijinsia bila kuathiri ubora wa mafunzo yanayotolewa,” alisema na kuongeza:


“Mafanikio haya yanathibitisha dhamira thabiti ya kuimarisha jeshi letu, hususan katika mafunzo ya mbinu za kijeshi na nidhamu. Chini ya uongozi wako makini, jeshi limeendelea kuwa imara na kutekeleza majukumu ndani na nje ya nchi. Leo tunapokabidhi maofisa wapya, ninakuhakikishia kuwa wako tayari kulitumikia taifa kwa ujasiri, uadilifu na kwa kuzingatia maono yako na kujitoa kwako kunakotia moyo katika kulinda amani na usalama wa nchi yetu.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha TMA Monduli, Meja Jenerali Jackson Mwaseba, alisema Jeshi litaendelea kuweka mazingira wezeshi na kutoa elimu bora itakayojenga uzalendo wa kweli na maadili kwa wanajeshi hao. Alisema kuwa kwa ujumla kulikuwa na wanaume 257 na wanawake 39.


Akizungumzia kundi la 06/22 la Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kijeshi, alisema lilifunguliwa Oktoba 24, 2022 likiwa na wanafunzi 155. Kati yao, 49 waliacha masomo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo maombi binafsi, kutofikia viwango vya kitaaluma, matatizo ya uaminifu, ugonjwa na utoro. Hivyo, wanafunzi 106 ndio waliohitimu mwaka huu.

Kwa kundi la Regular, alisema lilianza Desemba 20, 2024 likiwa na wanafunzi 173. Kati yao, 102 wamehitimu baada ya wengine 71 kushindwa kuendelea kutokana na sababu mbalimbali kama vile kukimbia mafunzo, maombi binafsi, kukosa uaminifu, ugonjwa, kutofikia viwango vya kitaaluma na kushindwa kuonyesha ufanisi.

“Nawapongeza wote waliofanya vizuri katika masomo, mazoezi na mitihani yao. Nawakumbusha kuwa JWTZ limefanya mambo mengi kuweka mazingira wezeshi kwao ili kutoa elimu yenye ubora kwa manufaa yao binafsi, kwa Jeshi na taifa kwa ujumla,” alisema na kuongeza:


“Ni matarajio makubwa ya taifa kuwa elimu waliyoipata itawajenga kuwa wazalendo wa kweli, watu wenye maadili mema na uwezo wa kupambanua changamoto mbalimbali kwa kuzingatia misingi ya haki na utu. Hivyo, mnayo dhamana kubwa ya kutumia taaluma yenu kutekeleza kwa vitendo malengo ya jeshi na taifa kwa ujumla.”

Awali, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Rhimo Nyansaho, amesema Wizara itaendelea kuhakikisha wanaongeza idadi ya wahitimu wanawake na kuwa maofisa hao wako tayari kutumikia nchi kwa ujasiri na uaminifu katika kulinda amani na usalama wa taifa.

Amesema kuwa hii ni mara ya tatu tangu Chuo hicho kilipoanza kujisimamia katika utoaji wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kijeshi.

Pia, Wizara itaendelea kuhakikisha idadi ya wanawake inaongezeka; wakati wa mahafali ya nne na tano, wanawake walikuwa 21, tofauti na mwaka huu ambapo idadi yao imeongezeka hadi 25, huku wanaume wakiwa 81.


“Mwaka huu imekuwa 25, japo ongezeko hili ni dogo ila Wizara inaendela kuchukua hatua mahsusi kuhakikisha idadi ya wahitimu wanawake inaongezeka mwaka hadi mwaka ili kuimarisha uwiano wa kijisia bila kuathiti ubora wa viwango vya mafunzo yanayotolewa,” amesema na kuongeza;

“Mafaniko haya ni uthibitisho wa dhamira ya dhati madhubuti kuimarisha jeshi letu, ikiwa ni pamoja na mafunzo mbinu za kijeshi na nidhamu chini ya uongozi wako makini jeshi letu limekuwa makini kutekeleza majukumu ndani na nje ya nchi.

“Leo tunapokabidhi maofisa wapya ninakuhakikishia kuwa maofisa hawa wako kutumikia nchi yao kwa ujasiri na uadilifu wakizingatia maono yako kujitoa kwako, usiotetereka katika kulinda amani na usalama wa taifa letu,” amesema.

Awali, Mkuu wa Chuo cha TMA Monduli, Meja Jenerali Jackson Mwaseba, amesema Jeshi litaendelea kuweka mazingira wezeshi na kutumia elimu yenye ubora itakayowafanya kuwa wazalendo wa kweli na wenye maadili ambapo kati yao wanaume walikuwa 257 na wanawake 39.


Mkuu huyo amesema kwa kundi la 06/22 la shahada ya kwanza ya sayansi ya kijeshi, yalifunguliwa Oktoba 24, 2022 ambapo walikuwa wanafunzi 155 kati ya hao 49 waliacha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo maombi binafsi, kutofikia viwango vya kitaaluma, uaminifu, ugonjwa pamoja na utoro, ambapo leo wamehitimu 106.

Kuhusu kundi la Regular amesema lilianza Desemba 20,2024 ambapo walikuwa 173 ambapo leo wamehitimu 102, kutokana na wengine 71 kushindwa kumaliza kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukimbia mafunzo, maombi binafsi, kukosa uaminifu, ugonjwa, kutofikia viwango vya kitaaluma na kukosa ufanisi.

“Nawapongeza wote waliofanya  vizuri katika masomo, mazoezi na mitihani yao, nawakumbusha JWTZ imefanya vitu vingi katika kuweka mazingira wezeshi kwao ili kutoa elimu yenye ubora kwa manufaa yao binafsi, Jeshi na taifa kwa ujumla,” amesema na kuongeza;


“Ni matarajio makubwa kwa taifa kuwa elimu waliyoipata itawasaidia kuwa wazalendo wa kweli, wenye maadili mema na kupambanua changamoto mbalimbali katika misingi ya haki na utu, hivyo mnayo dhamana kubwa kutumia taaluma zenu kutekeleza kwa vitendo malengo ya jeshi na taifa kwa ujumla,” amesema.