……….
Ma Mwandishi Wetu Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi kimemtaka aliyekuwa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman , iwapo chama chake kina ubavu wa kushindana na CCM kisubiri Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2030.
Aidha ,CCM kimeyaita madai ya kutaka Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar urudiwe huku OMO akiamini atamshinda Rais Dk Hussein Ali Mwimyi amesema hizo ni mbwembwe na maneno ya faraja kwa wafuasi wake.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanziabr Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis amesema hayo huku akimtaka OMO aachane na stori za Uchaguzi kwakuwa ukurasa huo umeshafungwa rasmi.
Mbeto alisema inashangaza kukisikia ACT kikidai kuwa kilishinda wakati wananchi wameshampigia kura Rais Dk Mwinyi ambaye sasa , anaiongoza Serikali na kujipanga kuleta maendeleo yatakayoonekana.
“Mwambieni OMO aache porojo badala yake aende ikulu akaape kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais. Ikiwa ameshindwa kazi awapishe wenzake washirikiane na Rais Dk Mwinyi kuiletea maendeleo Zanzibar ” Alisema Mbeto
Katibu huyo Mwenezi aliongeza kusema ACT kiache kuidanganya dunia badala yake kikubali ukweli nguvu za ushindi wa CCM zimetokana na haiba ya ustawi wa Maendeleo yanayoonekana hivi sasa Unguja na Pemba.
‘Ile zama ya kusambaza propaganda uchwara kupitia radio vifua na watu kuwadanganyana vibarazani imepita. Wananchi hawataki kushabikii siasa za chuki na migawanyiko ‘Alieleza
Mbeto alisema madai kuwa uchaguzi ukirudiwa tena Rais Dk Mwimyi hatapata kura asilimia 30,mbeto ameyaita hayo ni maneno yasioingia akili na kuaminika.
Alieleza kuwa kwa wakati huu hadithi za uchaguzi mkuu hazina nafasi hata ya kusikilizwa au kufuatiliwa na wananchi, badala yake watu wanaitarajia SMZ izidi kuongeza kasi ya mabadiliko kiuchumi, kisiasa na kijamii.
“Uchaguzi wa Mwaka 1995 wapo wakiodai Dk Salmim Amour ataondoshwa kabla ya Mwaka 200.Wakasema tena Dk Amani Karume hamalizi muda wake. Walipokataa kushirikiana na Dk Ali Mohamed Shein SUK iliundwa na kusongambele “Alisema Mwenezi huyo.