Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akizungumza na wanahabri akielezea kuhusu ziara ya program maalum ya Dar City Tour ambayo imefanyika jijini Dar es salaam.
Afisa Muhifadhi Kutoka Makumbusho ya Taifa Justine Nkungwe akiwaeleza wanahabari maeneo ya kihistoria wakati wa ziara ya program maalum ya Dar City Tour ambayo imefanyika jijini Dar es salaam.
Mhifadhi Mwandamizi Kijiji cha Makumbusho Wilhelmina Joseph akizungumza na wanahabari wakati wa ziara ya program maalum ya Dar City Tour ambayo imefanyika jijini Dar es salaam.
Afisa Utalii Makumbusho ya Taifa Kituo Cha Malikale kilichopo eneo la Mbuamaji Shukuru Thomas akiwaeleza wanahabari maeneo ya kihistoria wakati wa ziara ya program maalum ya Dar City Tour ambayo imefanyika jijini Dar es salaam.
……….,……
NA MUSSA KHALID
Shirikia la Makumbusho ya Taifa la Tanzania limejipanga kuendeleza utafiti wa urithi wa Taifa Ikiwemo kutangaza na kukuza utalii Ili kuvutia jamii na wageni wengi zaidi kutembelea na kujifunza historia katika Makumbusho hizo.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga wakati akizungumzia program Maalum ya Dar City Tour ambayo imefanyika tarehe 28/11/2025 katika maeneo mbalimbali ya kihistoria ikiwa na lengo la kukuza uelewa wa jamii juu ya umuhimu wa Makumbusho na Malikale.
Aidha amesema kuwa Jukumu la kukuza utalii na urithi wa Utamaduni ni la jamii nzima kwani inaakisi Moja kwa Moja malengo ya msingi ya Dira ya maendeleo ya Tanzania 2050 ambayo ni kujenga Taifa lenye kujiamini katika Utamaduni wake.
DKT Lwoga amesema kuwa pia Moja ya malengo yao ni pamoja na kuboresha miundombinu ya uhifadhi,Maonyesho na huduma za wageni,kuhifadhi urithi wa kidigitali na kuongeza upatikanaji wake na kuhamasisha na kushirikisha jamii mbalimbali Ikiwemo Halmshauri kuanzisha Makumbusho.
“Tanzania imejaaliwa urithi wa Utamaduni na Malikale adimu na WA kipekee duniani kuanzia visukuku(masalia) ya zamadamu vilivyogunduliwa huko Olduvai Gorge,urithi wa bishara za Karne za Mwambao wa Afrika Mashariki, historia ya ukombozi wa Afrika na uhuru wetu”amesema Dkt Lwoga
Awali akizungumza katika ziara hiyo,Afisa Muhifadhi Kutoka Makumbusho ya Taifa Justine Nkungwe amesema kuwa dhamira yao ni kuendelea kuongeza ushawishi wa kuwavutia watanzania pamoja na wageni Kutoka nje kutembelea kwa wingi katika Makumbusho na Malikale ili waweze kujionea urithi wa Taifa lao.
Kwa upande wake Afisa Utalii Makumbusho ya Taifa Kituo Cha Malikale kilichopo eneo la Mbuamaji Shukuru Thomas amezungumzia mji huo wa kale kuwa ulikuwa mji wa Kibiashara,huku Mhifadhi Mwandamizi Kijiji cha Makumbusho Wilhelmina Joseph ameeleza lengo la uwepo wa kijiji hicho ni kihifadhi urithi wa utamaduni.
Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu Makumbusho amewasihi wanahabari kuwa mabalozi wa kutangaza urithi wa Taifa ikiwemo kuwahamasisha watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi kufanya utalii katika Makumbusho na Malikale nchini.




