WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Riziki Pembe Juma, amesema ujenzi wa viwanja vya michezo ni hatua muhimu katika kuibua na kukuza vipaji vya vijana nchini.
Ametoa kauli hiyo jana Desemba 4, 2025 wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi wa viwanja vya michezo katika Wilaya za Unguja.
Waziri huyo amesema ujenzi wa viwanja hivyo unaendelea kwa kasi na vitatoa fursa kwa vijana kuendeleza vipaji vyao.
Hivyo ameahidi kusimamia upatikanaji wa vifaa muhimu ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ndani ya muda uliopangwa.
Naye, Kamishna wa Idara ya Michezo Zanzibar, Ameir Mohamed Makame, amesema usimamizi mzuri wa miradi hiyo utawezesha vijana kukuza na kuendeleza vipaji vyao.
Aidha, Kamishna Ameir ametoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu ya michezo ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali.
