Na Mwandishi Wetu
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeshika nafasi ya pili katika tuzo ya uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu kwa Viwango vya Kimataifa kwa mwaka 2024 kwa Mamlaka za Udhibiti zilizoshindanishwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu nchini (NBAA)
Tuzo hiyo imepokelewa na Mkurugenzi wa Fedha CPA Pascal Karoomba Mkurugenzi wa Fedha kwa niaba yaMkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya APC Bunju Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Fedha CPA Karomba wa amesema ushindi walioupata sio rahisi kwani taasisi ni nyingi lakini bado wameendelea kuwa na ubora huku wakijipanga katika kurudi katima nafasi ya kwanza.
Amesema TASAC imeendelea kuchukua ushindi katika nafasi mbambali katika Tuzo za NBAA katika kipengele cha Mamlaka za udhibiti.
Amesema ushindi huo unaonesha rasilimali walizopewa na majukumu unaonesha jinsi ambavyo wanawajibika katika utekelezaji wa majukumu yao ambapo wamekuwa wakiyafanya kwa weledi .

Wakiwa katika picha mara baada ya kutangazwa washindi wa pili Tuzo za NBAA.