Na Khadija Kalili, Kibaha
MEYA wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Nicas Mawazo amesema kuwa hawatamvumilia mtendaji ambaye atakwamisha maendeleo ya wananchi.
Dkt.Mawazo amesema hayo leo tarehe 3 Desemba 2025 alipoongea na Waandishi wa habari mara baada ya baraza la madiwani la Halmashauri ambalo lilimchagua kuwa Meya wa Halmashauri hiyo.
Amesema kuwa watumishi wakiwemo wakuu wa idara wasifanye kazi kwa mazoea waache badala yake wawatumikie wananchi wanataka kicheko kwa changamoto zao kutatuliwa.
“Tutawasemea wanyonge na hatutakuwa na huruma na mtendaji ambaye anakwamisha maendeleo na tutamchukulia hatua kwani tunataka tuwatumikie wananchi,”amesema Dkt.Mawazo.