Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasilisha rasmi ujumbe wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuelekea maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru yatakayofanyika kesho, Jumapili Desemba 09, 2025.
Amesema kuwa kwa mujibu wa maelekezo ya Rais, kesho itakuwa siku ya mapumziko ya kitaifa, hivyo Watanzania wanashauriwa kutulia majumbani na kuitumia siku hiyo kwa kutafakari historia, thamani, na tunu za uhuru wa taifa.
Waziri Mkuu amebainisha kuwa ni muhimu wananchi kuitumia siku hiyo kujenga umoja, kuenzi amani na kuendelea kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa wale ambao majukumu yao ya kikazi yanawalazimu kutoka, kama huduma muhimu kwa umma, wataendelea kutekeleza majukumu yao kama kawaida.
Amehitimisha kwa kuwatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya Uhuru na kuwasihi kuendelea kudumisha utulivu, mshikamano na uzalendo.
Related
