Jeshi la Polisi limetoa taarifa rasmi kwa umma leo Jumatano, Desemba 10, 2025, likielezea hali ya ulinzi na usalama nchini katika saa za asubuhi.
Katika taarifa hiyo, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa hali ya usalama imeendelea kuwa shwari katika maeneo yote, huku askari wakiendelea kufanya doria na ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao bila wasiwasi.
Polisi wamesisitiza kuwa wameimarisha ulinzi katika maeneo yenye msongamano wa watu, barabara kuu na mitaa ya mijini, ikiwa ni sehemu ya hatua za kutuliza hofu kufuatia taarifa na fununu mbalimbali zilizokuwa zikisambaa mtandaoni.
Aidha, Jeshi la Polisi limewahimiza wananchi kuendelea kuwa watulivu na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa pale wanapoona viashiria vyovyote vinavyoweza kuhatarisha amani.
Related
