Mgeni rasmi akikata utepea kuashiria uzinduzi wa zahanati hiyo
-Zahanati mpya yazinduliwa katika kijiji cha Mangucha
Ufanikishaji wa mradi huu ni moja ya utekelezaji wa mkakati endelevu wa kampuni ya Barrick unaojumuisha ushirikiano na wadau na vipaumbele ambao umelenga kufanikisha kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zinazoishi kwenye maeneo yaliyopo Jirani na migodi yake sambamba na kufanikisha utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Dunia (SDGs).
Akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano ya zahanati hiyo Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime, Albinus Kirina, alisema kukamilika kwa ujenzi wa zahanati ya Mangucha kutawaondolea wakazi 4,460 wa kijiji hicho adha waliyokuwa nayo ya kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya nje ya kijiji hicho.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara, aliitaka idara ya afya kutumia baadhi ya vyumba vya zahanati hiyo kwa ajili ya huduma za wanawake wanaojifungua wakati ujenzi wa majengo ya mama na mtoto na miundombinu ya kichoma taka yakisubiriwa.“Haitakuwa na maana kama akina mama hawatapata huduma za kujifungulia hapa,” alisema Mbunge Waitara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Matera Newland Chacha, naye aliushukuru Mgodi wa Barrick North Mara na kuahidi kuendelea kuupatia ushirikiano katika utekelezaji wa miradi mingine ya CSR ndani ya halmashauri hiyo.
Naye Diwani wa Kata ya Nyanungu, Tiboche Richard, aliishukuru Barrick North Mara kwa kuwezesha ujenzi wa zahanati hiyo ambayo imesogeza huduma za afya jirani na wananchi wa Mangucha.“Tunawashukuru sana watu wa Mgodi wa Barrick North Mara na tutaendelea kuwa mabalozi wazuri wa mgodi,” alisema Diwani Tiboche.
Francis Uhadi“Sekta ya afya ni ya pili kwa ukubwa wa uwekezaji wa CSR, ikiwa na asilimia 20 ya fedha zote tulizowekeza hadi sasa. Tangu mwaka 2020 hadi sasa, mgodi umewekeza shilingi bilioni 5.4 katika ujenzi wa zahanati, vituo vya afya, nyumba za watumishi na vifaa tiba.
“Kwa mwaka 2025, tunatekeleza miradi 21 ya afya yenye thamani ya shilingi bilioni 2.4. Miradi mingi ipo kwenye hatua za mwisho, ikiwemo huu wa Zahanati ya Mangucha uliokamilika kwa asilimia 100, na mingine itaendelea kukabidhiwa kwa halmashauri kadiri inavyokamilika.
“Makabidhiano ya zahanati hii ni ushahidi wa mafanikio tunayoyapata kupitia utekelezaji wa miradi ya CSR kwa ushirikiano wa karibu kati ya Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime pamoja na wananchi kwa ujumla,” alisema Uhadi.

Ripoti ya utekelezaji Mkakati Endelevu ya mwaka 2024 ya kampuni ya Barrick Mining Corporation iliyotolewa karibuni imebainisha mafanikio muhimu yaliyopatikana katika uendeshaji wa shughuli zake katika mataifa mbalimbali duniani.

Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Matera Newland Chacha akizungumza kwenye hafla hiyo
Afisa Mahusiano wa Barrick North Mara,Hermence Christopher akiongoza utaratibu wa ratiba katika hafla hiyo.
Sehemu ya wananchi wakiwemo viongozi wa serikali za vijiji kata ya Nyanungu
Katibu Tawala wa wilaya ya Tarime (DAS) Saul Mwaisenye akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya zahanati hiyo
Viongozi wakikagua jengo la zahanati hiyo










