Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Mipango, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo; Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso; Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga; Naibu Waziri wa Nishati; Menejimenti ya TISEZA pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge wakiwa katika ziara ya kukagua maendeleo Kongani ya Viwanda ya Kwala pamoja na kutatua changamoto, ziara hiyon imefanyika leo Desemba 10, 2025 Mkoani Pwani.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Mipango, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo; Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso; Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga; Naibu Waziri wa Nishati; Menejimenti ya TISEZA wakikagua maendeleo yaΒ Kongani ya Viwanda ya Kwala,Β Mkoani Pwani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Mipango, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari.
……….
Serikali kupitia Wizara mbalimbali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), imejipanga kuratibu uwekezaji wa viwanda 200 vyenye thamani ya shilingi trilioni 10, hatua inayotarajiwa kuleta manufaa kwa Taifa ikiwemo kuzalisha ajira 100,000.
Hatua hiyo imekuja kufuatia ziara ya viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais β Uwekezaji na Mipango, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo; Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso; Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga; Naibu Waziri wa Nishati; Menejimenti ya TISEZA pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge kutembelea Kongani ya Viwanda ya Kwala kwa lengo la kukagua maendeleo ya viwanda na kutatua changamoto zilizopo.
Akizungumza katika ziara hiyo leo, Desemba 10, 2025, katika Halmashauri ya Kibaha mkoani Pwani, Prof. Mkumbo amesema kuwa kwa sasa kuna viwanda 20 vinafanya kazi ambayo vimetoa ajira Kwa watu 2,000, huku akieleza kuwa lengo ni kufikisha viwanda 200 vitakavyotoa ajira 100,000.
Prof. Mkumbo amebainisha kuwa hadi sasa wawekezaji wamewekeza shilingi bilioni 625 na wanatarajia kuongeza uwekezaji hadi kufikia shilingi trilioni 10.
βTumekuja kukagua maendeleo ya viwanda pamoja na kutatua changamoto zilizopo. Tumeelezwa kuwepo kwa upungufu wa umeme ambapo kunahitajika megawati 100,β amesema Prof. Mkumbo.
Prof. Mkumbo amezitaja changamoto nyingine kuwa upungufu wa maji ambapo kunahitajika lita milioni 1.5 kwa simu, uhitaji wa kituo cha SGR kwa ajili ya usafirishaji wa uhakika wa bidhaa, pamoja na kutatua changamoto za kodi.
Prof. Mkumbo amesema kuwa ndani ya wiki mbili zijazo Serikali itaongeza megawati nne za umeme, pamoja na kuanzisha mradi wa kudumu wa usambazaji umeme kupitia ubia (PPP) wa kuleta umeme wa kilovolt 220 kutoka Chalinze, mradi wenye thamani ya dola milioni 67.
Imeelezwa katika mpango huo, wawekezaji watatoa fedha za ujenzi na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) litalipa gharama hizo kupitia mauzo ya umeme.
Katika upande wa maji, Waziri wa Maji, Mhe. Aweso, ameagiza kuletwa kisima cha maji pamoja na kupanga kutekeleza mradi wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 25 kupitia mfumo wa PPP.
Aidha, Prof. Mkumbo amebainisha kuwa Kongani ya Viwanda ya Kwala imepiga hatua kubwa, ikiwemo uwepo wa kiwanda cha kuzalisha vifaa vya nishati ya jua (Solar Power) kwa ajili ya soko la Marekani.
Kiwanda hicho kina thamani ya dola milioni 300, ambao kuna mpango wa kufikisha uwekezaji wa hadi trilioni mbili pamoja kujengwa kiwanda kikubwa cha kuzalisha chuma katika eneo hilo.