WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 11, 2025, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama, kilichotokea Itega jijini Dodoma.
Dkt. Mwigulu amesema taifa limepoteza kiongozi mstahiki na mtumishi wa umma aliyekuwa na historia ndefu ya kulitumikia Taifa kwa uadilifu, uzalendo na bidii.
Ametoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa, wananchi wa Peramiho na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msiba huo mzito.

Related
