ALUMANUS AWATAKA WADAU MBOZI KUHAMASISHA MICHEZO/ACHANGIA MIPIRA SHULE YA MSINGI WASA

:::::::::::

Wadau wa michezo wamehamasishwa kuendelea kuunga mkono sera ya michezo mashuleni hususani katika maeneo ya vijijini ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanajifunza kwa nadharia na vilevile wanapata muda wa kufanya michezo ili kuibua vipaji na kuimarisha afya zao

Rai hiyo imetolewa Wilayani Mbozi mkoani Songwe na Julius Mkwesera wakati akikabidhi mipira miwili kwa niaba ya Alumanus Mwasenga Mchambuzi wa Mpira wa Miguu TBC kwa shule ya msingi wasa lengo likiwa ni kuhamasisha michezo kwa wanafunzi mashuleni.

Akipokea mipira hiyo mwalimu mkuu wa shule ya msingu Wasa Josphat Njeje amewataka wadau wa michezo nchini kuunga mkono juhudi hizo ili kuwezesha upatikanaji wa vifaa vingi zaidi vya michezo huku baadhi ya wanafunzi wakiwashukuru wadau waliotoa mipira hiyo kwani itawasaidia katika kukuza vipaji shuleni hapo na kuimarisha afya zao