WATOTO WAWILI WATEKETEA KWA MOTO MOSHI.

WATOTO wawili wa miaka 4 na 2 wamefariki dunia baada ya moto kuteketeza nyumba waliyokuwa wakiishi katika Mtaa wa Katanini, Kata ya Katanini, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza nyumbani hapo, Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomaji amesema watoto hao kuwa ni Jerial Shayo (4) na Leoni Shayo (2) watoto wa wakili wa kujitegemea, Caessar Shayo.

” Watoto waliopoteza maisha ni Jerial Shayo(4) na Leoni Shayo (2) pia kulikuwa na majeruhi baba na mama wa watoto hao na kwa sasa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Kanda ya kaskazini KCMC,”aAlisema Kaimu Kamanda Zimamoto.

Kamanda Jeremiah amesema tukio hilo limetokea leo majira ya saa nne asubuhi, ambapo kwa mujibu wa mashuhuda, watoto hao walifariki dunia muda mfupi baada ya kupewa uji na dada wa kazi.