Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude, Tarehe 17 Desemba, 2025 kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amefunga rasmi Mkutano wa 18 wa Mapitio ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR), uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Akizungumza wakati wa hitimisho la mkutano huo, Mhe. Mkude ameipongeza Wizara ya Uchukuzi na Taaasisi zake, wadau wa kisekta na washirika wa maendeleo kwa majadiliano ya kina kuhusu mwenendo wa sekta ya uchukuzi na kuweka mikakati ya kuimarisha mfumo jumuishi wa usafiri nchini na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika miradi ya kimkakati ya uchukuzi ili kuongeza tija, ufanisi na ushindani wa uchumi wa taifa, sambamba na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 20
Ameeleza kuwa maazimio yote ya mkutano huo yaliyolenga kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya usafirishaji pamoja na kuimarisha mifumo ya TEHAMA yatafanyiwa kazi na Serikali kwa haraka
Aidha, amewataka wadau wa Sekta binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kuwekeza kwenye miradi ya usafirishaji nchini.
Katika hatua muhimu ya mkutano huo, Mhe. Mkude, kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, alizindua rasmi Mpango wa Utekelezaji wa Mazingira wa Sekta ya Uchukuzi (Transport Sector Environmental Action Plan – TSEAP 2025–2030), unaolenga kuhakikisha maendeleo ya miundombinu ya uchukuzi yanazingatia ulinzi wa mazingira na misingi ya maendeleo endelevu.
Naye, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. Godius Kahyarara, aliwasilisha tathmini ya utekelezaji wa miradi ya baadhi ya Taasisi za uchukuzi na wadau na kubainisha msimamo wa Wizara katika kuimarisha uratibu wa sekta ambapo alisisitiza kuwa maazimio yote 10 yamechukuliwa kwa uzito na yatafanyiwa kazi.
Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Tathmini na Ufuatiliaji, Bi. Devota Gabriel, aliwashukuru washiriki wote na kusema kuwa Mkutano wa 18 wa JTSR umefanyika kwa mafanikio makubwa, ukiwezesha tathmini ya kina ya changamoto, mafanikio na fursa zilizopo katika sekta ya uchukuzi, pamoja na kupokea mapendekezo muhimu kutoka kwa wadau wote.
.jpeg)
.jpeg)



.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

