TCAA yawahimiza Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege kuendelea Kuendana na Kasi ya Teknolojia

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi, amefungua Mkutano wa 26 wa mwaka wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania (TATSEA), huku akiwataka wahandisi hao kuendelea kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia katika sekta ya anga.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam, Bw. Msangi amesema kuwa kadri dunia inavyozidi kusonga mbele, mageuzi ya kiteknolojia katika mifumo ya uongozaji ndege yanaongezeka kwa kasi, hivyo ni muhimu kwa wahandisi wa Tanzania kubadilika na kukua sambamba na mwelekeo huo.

“Kadri siku zinavyokwenda, mabadiliko makubwa ya kiteknolojia yanazidi kushuhudiwa duniani. Hatuwezi kubaki tulipo ni lazima tuwe tayari kujiendeleza na kwenda na kasi ya dunia,” alisema Msangi.

Amesisitiza kuwa sekta ya usafiri wa anga ni nyeti na inategemeana na wadau wengi, hivyo ushirikiano baina ya vyama, taasisi na wataalamu wa fani mbalimbali ni muhimu katika kuongeza ufanisi na kuleta tija kwa Taifa.

Aidha, Bw. Msangi amekihimiza Chama cha TATSEA kuendelea kushirikiana na vyama vingine vya kitaalamu ndani na nje ya nchi ili kuongeza ubunifu, kubadilishana ujuzi na kuimarisha viwango vya usalama wa anga.

Kwa upande wake, Rais wa chama cha Wahandisi wa Mitambo ya kuongoza Ndege (TATSEA), Mhandisi Angela Kabali, amesema moja ya changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni kasi ya maendeleo ya kiteknolojia, hususan katika maeneo yanayohusisha akili mnemba (Artificial Intelligence – AI), ambayo imeanza kubadilisha mifumo ya kiufundi duniani.

Amesema mkutano huo wa 26 unatoa fursa kwa wataalamu kujadili namna bora ya kukabiliana na changamoto za teknolojia mpya, kuboresha mifumo, na kuongeza ulinzi wa mifumo ya uongozaji ndege nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akizungumza kuhusu namna Mamlaka hiyo ilivyojipanga kutoa mafunzo wa Wahandisi wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkutano wa 26 wa mwaka wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA) uliofanyika Desemba 19, 2025 Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akitoa neno kwenye Mkutano wa 26 wa mwaka wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA) pamoja na kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi.

Rais wa chama cha Wahandisi wa Mitambo ya kuongoza Ndege (TATSEA), Mhandisi Angela Kabali akizungumza kuhusu mikakati ya chama hicho iliyojiwekea pamoja na namna walivyojipanga kwenye Mkutano wa 26 wa mwaka wa TATSEA uliofanyika Desemba 19, 2025.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akimkabidhi tuzo Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi wa Mitambo ya Kuogozea Ndege, Mhandisi Zawadi Maalimu kwa niaba ya Mhandisi France Charle  iitwayo “Thorsten Were Award” ambapo Tanzania iliibuka mshindi

wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkutano wa 26 wa mwaka wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA) uliofanyika Desemba 19, 2025 Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akitoa zawadi kwa mwanachama mstaafu wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA) Yusuph Chonya wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Mwaka wa TATSEA uliofanyika Desemba 19, 2025.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akikabidhiwa zawadi na Rais wa chama cha Wahandisi wa Mitambo ya kuongoza Ndege (TATSEA), Mhandisi Angela Kabali wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Mwaka wa TATSEA uliofanyika Desemba 19, 2025.