WANAFUNZI 134 WA SHAHADA ,ASTASHAHADA NA SHAHADA YA UZAMILI WAJIUNGA NA VETA KWA MWAKA WA MASOMO 2026 8,000.00mm

…………..

Na Ester Maile Dodoma 

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya ufundi stadi (veta) imechagua wanafunzi 134 wenye elimu ya Astashahada, shahada na shahada ya uzamili ,ambapo 123 wamechaguliwa na 11 wanasubiria kupangiwa .

Hayo yamebainishwa leo Desemba 23 2025, na Mkurugenzi mkuu wa Veta CPA Anthony Kasore wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa kuchagua wanafunzi.

Aidha amebainisha kuwa kundi hilo baadhi ya masomo bebezi na mtambuka yaneondolewa kulingana na elimu waliyonayo ili kupunguza muda wa mafunzo na kuongeza ufanisi  

Hata hivyo katika jitihada za kuhakikisha kila mwananchi bila kujali elimu ,kazi au hali ya kimwili katika udahili anapata nafasi ya kujifunza CPA Kasore amesema veta imeondoa mtihani wa mchujo (Aptitude test) ilikuwezesha waombaji wengi zaidi kupata fursa kujiunga na vyuo vya ufundi stadi.