…………..
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameitahadharisha jamii ya watanzania kujiepusha na msukumo wa dhulma,uongo na ubinafsi unaoenezwa kupitia mitandao ya kijamii
Ametoa rai hiyo leo, wakati wa Ibada ya Krismasi iliyosaliwa katika Kanisa la Parokia ya Pwaga, wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma huku Paroko wa Parokia hiyo,Padri Daniel Kijaji akimuombea hekima na busara katika jukumu alilokabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan la kuiongoza wizara hiyo ambapo pia alimshukuru kwa kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni Kumi kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hilo.

.jpeg)
