Takriban watu wanane waliuawa na 18 kujeruhiwa katika mlipuko katika msikiti wa Ali Bin Abi Talib – mahali pa ibada ya jamii ya wachache ya Alawite – katika kitongoji cha Wadi al-Dahab.
Syria imekuwa katika njia ya mpito ya kisiasa tangu kupinduliwa kwa utawala wa Assad Desemba mwaka jana lakini inaendelea kukabiliwa na ghasia za kidini na nyinginezo.
Kundi linaloitwa Saraya Ansar al-Sunna limedai kuhusika, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.
Wito wa haki
“Katibu Mkuu anakariri kwamba mashambulizi dhidi ya raia na maeneo ya ibada hayakubaliki. Anasisitiza kwamba waliohusika lazima watambuliwe na kufikishwa mahakamani,” kauli alisema.
Pia “anatambua kwamba mamlaka ya Syria yamelaani shambulio hilo na kuthibitisha dhamira ya Serikali ya kupambana na ugaidi na kuwawajibisha wahusika.”
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alituma salamu za rambirambi kwa familia za waliouawa na kuwatakia waliojeruhiwa haraka na ahueni kamili, taarifa hiyo ilihitimisha.