JAS yafanya kikao cha kufunga Mwaka 2025

Na Mwandishi Wetu  Morogoro 27 Disemba, 2025.

Jumuiya ya Wanafunzi ya Jiba Active Students (JAS) imefanya kikao maalum cha kufunga shughuli za Mwaka 2025, kikao kilicholenga kufanya tathmini ya utekelezaji wa mipango, kujadili mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zilizojitokeza katika kipindi cha mwaka mzima pamoja na kuweka mipango ya kipindi kijacho.Akizungumza leo 28 Disemba, 2025.katika kikao hicho, viongozi wa JAS wakiongozwa na Mwenyekiti Sheikh,Dkt. Abdi Kassim Jiba, wamesema mwaka 2025 umekuwa na mafanikio makubwa hususan katika kuimarisha mshikamano wa wanachama, kushiriki shughuli za kijamii, kielimu na kujitolea, pamoja na kuongeza ushiriki wa wanachama katika programu mbalimbali za maendeleo binafsi na ya jamii.

Aidha, kikao hicho kilitoa fursa kwa wanachama kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha utendaji wa jumuiya hiyo katika mwaka ujao. 

Baadhi ya wanachama walipongeza uongozi kwa uwazi na ushirikishwaji, huku wakisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha nidhamu, ubunifu na mshikamano.

Katika hitimisho la kikao, JAS iliahidi kuingia Mwaka 2026 kwa nguvu mpya, mikakati madhubuti na dhamira ya kuendelea kuwajengea wanafunzi uwezo wa kitaaluma, kijamii na kimaadili kwa manufaa ya jamii kwa ujumla.