Dar es salaam. Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Bangladesh, Khaleda Zia amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.
Khalenda Zia aliyekuwa Waziri Mkuu wa taifa hilo kwa vipindi tofauti kuanzia mwaka 1991 aliondoka madarakani mwaka 2024, kufuatia shinikizo la waandamaji wakiwemo wanafunzi wakimtuhumu kwa ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
Taarifa kutoka uongozi wa chama cha upinzani nchini humo ambacho ni chama chake cha Bangladesh Nationalist Party (BNP), imeeleza kuwa kiongozi huyo amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya moyo na ini.
Imeelezwa kuwa Khaleda aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa Bangladesh na mwanamke wa pili pekee kuongoza serikali ya kidemokrasia ya taifa lenye Waislamu wengi baada ya Benazir Bhutto, alikwenda mjini London nchini Uingereza mapema mwaka huu kwa matibabu kabla ya kurejea nchini kwake.
“Madaktari wake walisema kwamba alikuwa na ugonjwa wa ini ulioenea, yabisi kavu, kisukari, na matatizo ya kifua na moyo.”imeeleza taarifa hiyo.
Kiongozi huyo alitambulika kama mtu mwenye kujitolea katika kipindi cha uongozi wake licha ya kuhukumiwa adhabu ya kifo Novemba mwaka huu, kwa tuhuma za ukandamizaji mbaya dhidi waandamaji hususani wanafunzi.
Akidaiwa kutumia nguvu kubwa kuwadhibiti kwenye maandamano yaliofanyika tangu Agosti 2024, kutokana matumizi mabaya ya madaraka na ufisadi na kusababisha kuondolewa madarakani kwa kiongozi huyo, hali iliyoliingiza taifa hilo katika mfumo wa serikali ya mpito inayoongozwa na Muhammad Yunus, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel.
Kiongozi huyo pia atakumbukwa kama mbadilishaji wa mfumo wa urais na wa bunge, katika kipindi cha uongozi wake ambapo aliondoa vikwazo kwenye uwekezaji wa kigeni na kufanya elimu ya msingi kuwa ya lazima na ya bure.
